Free Web Hosting Provider - Web Hosting - E-commerce - High Speed Internet - Free Web Page
Search the Web


Welcome To Bongo Explosions !
  Home Page | My Biography | My Photo Gallery | My Journey Abroad | Contact Me | My Favorite Links | Sign My Guest Book | My Shopping Store | East Africa Bongo Explosions  

TID na Naziz.....Watasema sana kideoni mwaka huu...haaaa!!

Msanii wa muziki wa kizazi kipya katika miondoko ya R&B ambaye alitingisha ndani ya Afrika Mashariki na Uingereza hivi karibuni na ambaye kwa sasa anatesa katika redio mbalimbali na 'songi lake' la Watasema Sana hivi karibuni anatarajia kufyatua video ya wimbo huo.
Akizungumza na mtandao wa Darhotwire juzi msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Khalid Mohammed alisema kutoka kwa video hiyo ambayo imerekodiwa na kampuni ya Paparazzi ya Jijini Dar es Salaam kutakuwa ni mwendelezo wa mpango wake wa.....

Gonga kujua zaidi


Super Star wa Wiki TID

Super Star wetu wa wiki ni Kijana Maarufu sana kwa sasa kutoka Jiji Kuu la Dar es Salaam nchini Tanzania.Anavuma na vibao vyake vikali kama Mpenzi Zeze na GirlFriend........Hivi sasa anatisha sana East Africa nzima kubali usikubali mimi kijana huyu namkubali sana

  Tuma Wazo/Maoni

Nawafagilia 'wazee' Prof Jay na King Crazy GK 'Bokasa'
C mcehzo ndugu zangu tutake tusitake hawa wazee wanatisha kinoma katika fani, hata kama wakisema muziki wa kizazi kipya unashuka lakini wazee hawa bado wamesimama, kwa upande wa Jay yeye nampa pongezi za dhati kwa kwa kitu chake cha Msinitenge sio siri kitu kimetulia na kinaonyesha wazi jinsi Jay alivyosimama katika fani, kwa upande wa GK na wenzake wa East Coast nawapa pongezi zangu kwa kitu chao cha Ama Zako ama Zangu, c mchezo masela wangu kitu bomba sanasana video yenu, Bip Up Wazee....

-  Josh, Kijitonyama - Tanzania

Kamata Explosions Zimeongoza 15th Sep - 02nd Jan
Jay mo ft. mangair - cheza kwa step
Bw Misosi ft. Mangair - nitoke vipi
Mangair ft. Dully - napokea simu
Mandojo & Domokaya - Nikupe
Wandago ft mangair - maisha ya mademu
Inspector Haroun - Byebye
Madii ft. Mandojo - kazi ya mola
Chief Rumanyika  - Fagilia
UVC  ft. maze b - wananichunia
Juma Nature - Salio la verse
Mandojo & Domokaya - Bongo Fiesta
Mack D ft. JUma Nature - Tabibu
TID feat. Jay Mo, Naziz, Wyre - Burudani 

DarHotWire Website

LYRICS ZA KIBONGO
MSANII : INSPECTOR HAROUN
WIMBO : ASALI WA MOYO 


Kiitikio
Wewe ndiye asali wangu wa moyo
Kwa dhiki na faraja mpenzi kaza roho
Ingawa watasema mengi midomoni mwao
Usiwajali hao!!

Verse 1

Hizi tenzi madhubi kalili thabiti mahususi
Kwako mpenzi swali liko wazi toka enzi
Sio siri tena sibabaiki 'aeiou' hapana
Sina kigugumizi tena domo sio gundi tena
kinywa chepesi murua laini
maridadi kabisa maneno natema
uuhfh!! haaah nashusha pumzi na hema
Mwana wa kahena nimekufa kimahaba
Unanichanganya kimahaba 
unanichanganya kwa mambo mengi kisura
kiumbo mshobo kama mpaka uroda
Najua wanakutazama kwa jicho la husda dada
Mtoto kichugwa kipoda tena bombaa
Ni wao tu roho zao za choyo wewe ndio asali wa moyo
Sintojali waniite zoba nimerogwa ama poyoyo
Wanataka kuzua mkumumba na jakamoyo
Hutu tuneno tudogodogo tusikupe 
shaka sana twende bega kwa bega
Kama samaki na maji 
Mizizi na ardhi tuzidi kuwachanganya.

kiitikio

Verse 2

Ewe ndiwe asali wa moyo wangu
Wanyuma yako wote nawaona machangu
Kwangu kwangu nakupa shahada yauvumilivu
Kwa wako utulivu sogea na utulize zetu mbivu

Woow! honey crazy! i cant bealive 
Nilipoanza kukutokea kukufukuzia
Wanaa walianza kupaka tena kukandia
aaah! hawezi kung'oa mtoto high class
Yaani mgumu kama kisiki hang'oleki hata kwa leki
kwanza hali yangu duni halafu nikijicheki
sina 'Usponi town' kwetu 
chai rangi vitumbu andazi 
Nyumba mbavu za mbwa aliye nje anatuona waziwazi 
Wakati shori kwao mambo ya mshiko , midikodiko
Chai ziwa juice passion,embe miwa 'rost' maini
tambi,kolonya, laini laini shata shata
nini shaka na vyapati vyapati 
Aaaaha eti ningempata wapi?
Mh!! iwe bojo kaisii nikwenda muno
Akanana kange ninkashaha engozi
wanga wameuwawa mtaani
ngebe zimezimwa mchuchu
Kuvinjari nami
Kila tozi atakae mtokea anamuona kama Osami
Unajua wengi hawajui maana ya kupenda
Unajuwa wengine wanaona uchafu hata kulamba denda
Unajua wengine wanaona hofu kukashifiwa kwa kuwatokea watoto
wa matajiri au uwoga wa kupigwa kalenda
Na wangejua mapenzi hayachagui fukara wala 
mtawala,dini, kabila desturi mila mradi
mmependana kama na B wangu tumeshibana

Rudia Kiitikio

Mtaa FM Website !


Binamu
 Toleo Lijalo ni albamu mpya ya msanii Mwana FA ambayo kwa sasa imekuwa gumzo katika soko la muziki wa kizazi kipya kwa kuwa na nyimbo moto moto kama Alikufa kwa Ngoma na Wanapendana pamoja na nyingine nyingi bombaaa..je wewe umeikosa? usikubali nenda kanunue usiikose....!!


'Mike T kumng'arisha dada yake kideoni....!

Msanii maarufu wa muziki wa hiphop, Mike T kutoka Iringa hivi karibuni naye ataungana na wasanii wengine ambao kwa sasa wamejikita katika kutengeza video za nyimbo zao mpya.Akizungumza na mtandao wa Darhotwire msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Mike Mwakatundu alisema video hiyo ya wimbo wake mpya wa Nibeep Baby anatarajiaha.........
Gonga kujua zaidi